Al’Imam Al’Mahdi Nasser Muhammad Al’Yamani
الإمام المهديّ ناصر محمد اليمانيّ
24 - ربيع الآخر - 1445 هـ
08 - 11 - 2023 مـ
04:33 صباحًا
(Kulingana Na Taqwimu Rasmi Ya Umul Qura)
(بحسب التّقويم الرّسميّ لأم القُرى)
__________


نَصَرَ اللهُ جَيشَ المُؤمِنين لتَحرِيرِ فلسطين بِخَمسَةِ آلافٍ من المَلائكةِ مُسَوِّمِينَ ..
Mungu ameipa ushindi jeshi la waumini kuikomboa Palestina kwa malaika elfu tano Kwa Vifaa vya kuvunja na kuvamia katika shambulio ..



Bismillah Al’Wahid Al’Qahar; Aliwashinda waovu washari (makomandoo) wakuvunzi waliofundishwa na Wazayuni na kutoka sehemu mbalimbali za ulimwengu kwa malaika elfu tano, waliohesabiwa au zaidi, kama Mungu apendavyo, kutoka kwa askari wake; Wakali na wenye nguvu zaidi kuliko wahalifu, walinzi wa mashetani, katika vita vya Gaza tukufu na katika vita vingine vya waumini, Ahadi ya Mwenyezi Mungu kwa Waumini wenye subira ambao wanapigania haki kwa ajili yao wenyewe, dini yao, ardhi yao, na utakatifu wa Mwenyezi Mungu; Mwenyezi Mungu hawapendi wachokozi, na Mwenyezi Mungu ana askari wa mbinguni na ardhini wa kuwaunga mkono wachamungu dhidi ya wavamizi. Sunnah za Mungu katika wa mwanzo na za mwisho; Hivi ndivyo tunavyowalipa wafanyao wema katika kila wakati na mahali. Mungu havunji ahadi yake. Kusadikisha Kauli Ya Allah Ta3ala:
{بَلَىٰ ۚ إِن تَصْبِرُوا وَتَتَّقُوا وَيَأْتُوكُم مِّن فَوْرِهِمْ هَٰذَا يُمْدِدْكُمْ رَبُّكُم بِخَمْسَةِ آلَافٍ مِّنَ الْمَلَائِكَةِ مُسَوِّمِينَ ‎﴿١٢٥﴾‏ وَمَا جَعَلَهُ اللَّهُ إِلَّا بُشْرَىٰ لَكُمْ وَلِتَطْمَئِنَّ قُلُوبُكُم بِهِ ۗ وَمَا النَّصْرُ إِلَّا مِنْ عِندِ اللَّهِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ ‎﴿١٢٦﴾‏ لِيَقْطَعَ طَرَفًا مِّنَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَوْ يَكْبِتَهُمْ فَيَنقَلِبُوا خَائِبِينَ ‎﴿١٢٧﴾}
Sadaqa Allah Al’3adhim:Sura[Al-imran:125/126/127].

Na jueni enyi jumuiya ya jeshi la waumini kuikomboa Palestina takatifu, enyi “Tufan Al’aqsa” mafuriko ya Msikiti wa Al-Aqsa. Kwa hiyo jua kwa uhakika kwamba ikiwa Mungu angekupa malaika bilioni tano wanaoandamana na ulinzi, au sawa nao, waliopangwa kupenya wakati wa mashambulizi, basi jueni na tena basi jueni kwamba ushindi unatoka kwa Mungu. Malaika ni watumishi wa Mwenyezi Mungu, askari wa Mwenyezi Mungu, walinzi wa waumini katika maisha ya dunia na akhera (waja wa Mungu kama nyinyi). Mwenyezi Mungu hakuwajaalia ila ni bishara njema kwa Waumini, ili zipate kutuza nyoyo zao kwamba Mwenyezi Mungu yu pamoja nao, na kwamba ushindi unatoka kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hikima.
Kwa hiyo shikamaneni na Mungu peke yake na mwombe Mungu peke yake. Neema Almawula Wa Neema Alnasir, Na hata ikiwa hamukuwaona Malaika Kwa Vifaa wanaokuja na nyinyi mara tu baada ya kuwashambulia maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui wenu, lakini wao Ma’Aduwi wanawaona kwa macho yao wenyewe wanapowakamata na kuwaua kwa ukatili. hakika sisi ni wakweli.

Tunamwambia Netanyahu, na askari wake, na watiifu wao wote: Kueni kwa ghadhabu yenu, ninyi nyote.

Wa Ya Subhan Allah Al’3adhim! Vipi na mimi nawasikia walinzi wa mashetani wakijadiliana ni nani atakayetawala Gaza tukufu baada ya ukandamizaji wa askari wa Hamas na makundi ya mukawama ya heshima?! Ni ajabu iliyoje enyi watu wasiokua warabu na Waarabu! Wanawezaje kusema hivyo, wakijiamini wenyewe, kwa kiburi na kujighuri kwa nguvu zao?!
Kana kwamba ushindi umetoka kwao wenyewe, na hawakumthamini Mwenyezi Mungu kama anavyostahiki, lakini Mwenyezi Mungu yu pamoja na watu wema, na ushindi unatoka kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hikima. Ametukuka Subhanahu Wata3ala 3uluwan Kabiran, Na Naapa Kwa Qasam Billah Al’Wahid Al’Qahar Lau askari wa Gaza yenye heshima, mashetani wote wa kibinadamu, wangekusanyika pamoja na majeshi yao yote na vifa zao zote za kijeshi, wasingeweza kuwashinda, na pamoja nao yuko Mungu Al’Wahid Al’Qahar; Hakuna awezaye kuwashinda, Kusadikisha Kauli Ya Allah Ta3ala:
{إن يَنصُرْكُمُ اللَّهُ فَلَا غَالِبَ لَكُمْ ۖ وَإِن يَخْذُلْكُمْ فَمَن ذَا الَّذِي يَنصُرُكُم مِّن بَعْدِهِ ۗ وَعَلَى اللَّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ ‎﴿١٦٠﴾‏}
Sadaqa Allah Al’3adhim:Sura:[Al-imran:160].

Hizi ni miongoni mwa sheria za Mwenyezi Mungu katika Kitabu. Ahadi kutoka kwake kwa wale wanaojitahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu katika kujilinda nafsi zao na dini yao ya kweli. Kusadikisha Kauli Ya Allah Ta3ala:
{وَكَانَ حَقًّا عَلَيْنَا نَصْرُ الْمُؤْمِنِينَ ‎﴿٤٧﴾‏}
Sadaqa Allah Al’3adhim:Sura:[Al-Rum:47].

Au hamjui kwamba mimi Ni Khalifa wa Mwenyezi Mungu, Mahdi Nasser Muhammad Al-Yamani, iliitangulia fatwa yangu kwa haki: Kwamba Wanaume wanaouzunguka Msikiti wa Al-Aqsa ni watu waaminifu kutoka katika harakati ya Hamas na wale wanaowaunga mkono kutoka katika makundi ya mukawama yaliyo waaminifu huko Palestina. Niliwachukua kua mawali, na wao ndio pekee ambao sikungojea “Beyaa” kutoa kiapo cha utii kwao; kwa kua wao Wametoa beyaa kwa Allah “Kwa sababu wanaweka kiapo cha utii kwa Mungu”, Walijitwika jukumu la kuitetea na kuulinda Msikiti wa Al-Aqsa, na kwa hiyo miaka kumi na minne iliyopita nilitangaza uaminifu wangu kwao. Nilitangaza kwamba mimi ni Kalifa wa Mwenyezi Mungu, Mahdi Nasser Muhammad Al-Yamani, mwaminifu kwa wale wanaowaunga mkono na kuwafanyia uadui wale wanaowafanyia uadui. Sina maskitiko kwao ili wanidhihirishe kwa walimwengu; Hakika Mwenyezi Mungu ndiye atanifanya nionekane juu ya wanadamu wote kwa adhabu kali kutoka kwa Mwenyezi Mungu katika usiku wa kutokea kwa nyota ya Saqr mupende musipende, na mutajua kwamba Mwenyezi Mungu ameikamilisha nuru yake hata kama wahalifu huchukia kutokea kwake.

Ingawa Mungu anamsaidia mja wake pamoja na askari wake wote katika ufalme, lakini mimi nashuhudia kwa Mungu, ushuhuda ambao utandikwa Ju yangu na Mola wangu: Ushindi unatoka kwa Mwenyezi Mungu, jambo limetoka kwa Mwenyezi Mungu, na kwa Mwenyezi Mungu mambo yote yanarejeshwa. Anajua udanganyifu wa macho na yale yanayo fichwa vifuani. Neema Almawula Wa Neema Alnasir.

Na Salam Ju Ya Mitume na Alhamdulillah Rabil3alamin..
Khalifa Wa Allah Ju Ya Ulimwengu Wote (Bara Yake Na Bahari Yake) Al’Imam Al’Mahdi Nasser Muhammad Al’Yamani.
خليفةُ اللهِ على العالَم بأسرِه (برّه وبحره) الإمام المهديّ؛ ناصر محمد اليمانيّ.
___________